Jumamosi 28 Juni 2025 - 13:44
Iran imeivuka kwa nguvu njama za kimataifa na kufikia zama mpya za uimara

Hawza/ Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, amezungumzia ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni na Marekani, na ameuita kuwa ni hatua ya mabadiliko katika historia ya muqawama na mlingano wa kisiasa ktika ukanda huu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Al-Haj Amin Abu Alaa al-Wala'i, Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa siku za Ashura na matukio ya hivi karibuni katika ukanda huu, huku akitoa mkono wa pole kwa mnasaba wa maombolezo ya Bwana wa Mashahidi, Imam Husein (as), alizungumzia ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni na Marekani, na akauelezea kuwa ni hatua muhimu ya kihistoria katika njia ya muqawama na katika mlingano wa kisiasa wa eneo hili.

Akiitaja Ashura kuwa ni chanzo cha msukumo wa muqawama na uhuru, na kwa kuashiria mashambulizi ya hivi karibuni ya Wazayuni, alisema kwamba: Vikosi vya muqawama viliingia kwa ushujaa uwanjani na vikamlazimisha adui kurudi nyuma na kuvuruga kabisa hesabu zake zote potofu. Adui, akiwa na dhana ya kumiliki uwezo wa kuishinda Iran kwa urahisi, alianzisha vitimbi, lakini alikutana na uhalisia wa nguvu ya Iran.

Kwa mujibu wake, kukubali kwa Marekani na utawala wa Kizayuni kusitisha vita ni ushahidi wenyewe kwamba hawakuwa na matumaini yoyote ya ushindi, na mbele ya nguvu ya Iran hawakuwa na njia nyingine isipokuwa kusitisha mapigano.

Abu Alaa al-Wala'i, kwa kusisitiza kuwa Iran kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu itakuwa nchi ya nyuklia yenye malengo ya amani, na kwamba mipango yote ya Magharibi kwa ajili ya "Mashariki ya Kati Mpya" itashindwa, alibainisha: Maadui wanapaswa kuwajibika kutokana na hasara zote na madhara ya vita hivi.

Akiashiria nafasi ya uongozi wenye hekima wa Imam Khamenei na ushirikiano wa watu wa Iran, alisema: Msaada huu wa wananchi – licha ya jitihada zote za kuzua machafuko ya ndani – ulikuwa ni mojawapo ya nguzo muhimu za ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu wa Kataib Sayyid al-Shuhada alibainisha kuwa: Iran si nchi tu, bali ni mradi mkubwa wa ustaarabu ambao hauwezi kusitishwa kwa mauaji ya kisiasa au kwa kumuondoa mtu binafsi. Iran imeibuka na ushindi kutoka katika njama za kimataifa, na leo hii ni imara na yenye mshikamano kuliko wakati wowote ule.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha